Sakata la Uingereza Kujiondoa EU.

Mjumbe wa Umoja wa Ulaya anayesimamia mchakato wa BREXIT amesema jumuiya hiyo bado inasubiri mapendekezo kutoka kwa waziri mkuu Boris Johnson ili kuumaliza mkwamo kuhusu suala la nchi hiyo ya Uingereza kujitowa katika Umoja huo,hatua ambayo inatakiwa kuchukuliwa kufikia mwishoni mwa mwezi ujao wa Oktoba.

Michel Barnier amewaambia waandishi habari kwamba bado Umoja wa Ulaya upo tayari kuyaangalia mapendekezo ya Uingereza.

Mjumbe wa Boris Johnson kuhusu suala hilo David Frost amekuwa akifanya mazungumzo mjini Brussels wiki hii lakini hakuna kilichofikiwa hadi wakati huu.

Waziri mkuu Johnson anataka kipengee kinachohusu mpaka wa Ireland kiondolewe kwenye makubaliano ya Brexit yaliyofikiwa baina ya viongozi wa Umoja wa Ulaya na mtangulizi wake,Theresa May.

Comments

comments

clement

Read Previous

VIDEO: Rais Dkt. Magufuli akiendesha Gari la jeshi.

Read Next

Upigaji wa Kura za Kuchagua wenyeviti wa Serikali za Mitaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!