Spika amuonya Johnson kwa Kutoheshimu Sheria.

Spika wa bunge la Uingereza John Bercow amemuonya waziri mkuu Boris Johnson kuhusu kutoheshimu sheria kwa kukataa kuomba kusogezwa mbele muda wa nchi hiyo kujitoa Umoja wa Ulaya ama Brexit.

Spika huyo ameapa kupinga jaribio lolote linalonuia kulikwepa bunge. Kulingana na shirika la habari la Press Association la Uingereza, spika huyo wa bunge amesema kutoheshimu sheria kunaweza kuwa ni mfano mbaya kabisa utakaoonyeshwa mbele ya umma.

Bercow ameonya kwenye hotuba yake jijini London kwamba iwapo serikali itakaribia kufanya hivyo bunge litatumia nguvu zake zote kuondoa uwezekano huo.

Matamshi yake yanakuja baada ya waziri mkuu Johnson kukanusha shutuma kuwa alimdanganya Malkia Elizabeth kuhusu kuomba kuvunjwa bunge mwezi huu.

Bunge, mapema mwezi huu lilipitisha sheria iliyolenga kuzuia Brexit bila ya makubaliano ingawa Johnson anasisitiza kuondoka kama ilivyopangwa awali Oktoba 31, kwa makubaliano ama bila ya makubaliano.

Comments

comments

clement

Read Previous

Sintofahamu kuhusu atakapozikwa Marehemu Mugabe.

Read Next

Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC , ajiuzulu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!