Wananchi wa Tunisia, wanasubiri matokeo ya mshindi wa uchaguzi wa Urais

Wananchi wa Tunisia, wanasubri matokeo ya mshindi wa uchaguzi wa urais baada ya kupiga kura mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo karibu nusu ya wapiga kura walijitokeza kushiriki katika uchaguzi huo wa pili tangu kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani Ben Ali katika maandamano ya wananchi mwaka 2011.

Wagombea 26 wakiwemo wanawake wawili wanawania wadhifa huo ambapo Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa wikik hii. Wagombea hao ni pamoja na mfanyabiashara Nabil Karoui, ambaye yuko kizuizini kwa kesi ya utakatishaji wa fedha, na Kais Saïed, ambaye ni mgombea binafsi.

Wakati hayo yakijiri Mjane wa rais wa zamani wa Tunisia Beji Caid Essebsi amefariki dunia wakati nchi hiyo inafanya uchaguzi wa urais ulifanyika hapo jana.

Taarifa iliyotolewa na Mtoto wa Essebsi, Hafedh Caid Essebsi ameeleza kwamba mama yake, Chadlia Saida Essebsi amefariki akiwa na umri wa miaka 83 ambapo alikuwa akisumbuliwa na maradhi.

Mwishoni mwa mwezi Julai, Chadlia aliwapokea viongozi kadhaa wa kimataifa waliokwenda kumpa pole baada ya kifo cha mumewe ambaye alikuwa kiongozi wa taifa hilo.

Comments

comments

George Ambangile

Read Previous

Wizara imesesma ipo katika mchakato wa kusanifisha Lugha ya alama.

Read Next

Mauzo katika soko la hisa la Dar es Salaam imepanda wiki iliyopita kutoka Shilingi Milioni 81.66 hadi kufikia milioni 184. 40 .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram