Rais Abdel Fattah al Sissi wa Misri amekutana na waziri mkuu aliyeteuliwa hivi karibuni wa Sudan

Rais Abdel Fattah al Sissi wa Misri amekutana na waziri mkuu aliyeteuliwa hivi karibuni wa Sudan Abdallah Hamdok kabla ya kuelekea jijini New York kuhudhuria mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya Rais mjini Cairo, viongozi hao wawili wamezungumzia uhusiano wa pande mbili.

Ushirikiano kati ya majirani hao wawili wanaopakana na mto Nile umedhoofika kutokana na mivutano ya hapa na pale wakati wa utawala wa miongo mitatu wa rais wa zamani Omar al Bashir.

Misri inategemea kufungua ukurasa mpya tangu Rais wa zamam Al Bashir alipotimuliwa madarakani na wanejeshi mwezi April jana.

Comments

comments

clement

Read Previous

Wananchi 69,000 kupata Umeme kupitia Mardi wa ujazilizi awamu ya pili.

Read Next

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amemtolea wito mpinzani wake mkubwa Benny Gantz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!