Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran kufuatia mashambulio katika visima vya mafuta vya Saudi Arabia.

Katika maelekezo yake Rais Trump amemtaka waziri wake wa Fedha Steven Mnuchin ahakikishe vikwazo hivyo vinakuwa vikali zaidi ya vile vya awali ingawa vielelezo vya vikwazo hivyo bado havijulikani.

Rais huyo wa Marekani amesema uwezekano wa kujibu shambulizi hilo kijeshi ni njia ya mwisho hivyo taifa hilo lisijione kana kwamba linaogopwa.

Bado pande hizo mbili zinazohasimiana zinaendelea kubishana kuhusu nani walikuwa nyuma ya mashambulio dhidi ya vinu vya mafuta vya Saudi Arabia.

Waasi wa Houthi nchini Yemen wanadai walihusika na mashambulio hayo ingawa Marekani inailaumu Iran kuwa nyuma ya mashambulio hayo.

Comments

comments

George Ambangile

Read Previous

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amemtolea wito mpinzani wake mkubwa Benny Gantz

Read Next

Waziri mkuu Kassim Majaliwa Kassim amefungua mkutano wa wakuu wa Polisi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram