Serikali ya Uingereza imejitetea mbele ya Mahakama ya juu.

Serikali ya Uingereza imejitetea mbele ya mahakama ya juuya nchi hiyo, ikisema uamuzi wa waziri mkuu Boris Johnson kuahirisha vikao vya bunge wiki chache tu kabla ya nchi hiyo kujitoa katika Umoja wa Ulaya, ilikuwa sawa na haikuenda kinyume na sheria.

Leo ni siku ya pili katika siku tatu ambazo mahakama inasikiliza kesi hiyo ya kihistoria inayoweka kwenye mizani nguvu ya bunge na mamlaka ya serikali, wakati ambapo tarehe ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya Oktoba 31, ikikaribia na kuleta mihemko ya kiuchumi na kisiasa.

Wakili wa serikali James Eadie amesema kuwa mahakama ya chini ilikuwa sahihi kuamua kwamba uamuzi wa Johnson ulikuwa suala la juu kisera na kisiasa na si kisheria.

Wapinzani wa serikali wanahoji kuwa Johnson aliahirisha vikao vya bunge kinyume na sheria, kwa malengo yasiyo sawa ya kuwazuia wabunge wasijadili mipango yake ya Brexit.

Pia wanamshutumu Johnson kwa kumdanganya Malkia Elizabeth wa pili ambaye idhini yake rasmi ilihitajika kwa bunge kuahirishwa.

Comments

comments

clement

Read Previous

Waziri Jafo awataka Viongozi kutekeleza Majukumu yao.

Read Next

Madhara ya Kuzagaa kwa bidhaa Bandia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!