Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amemtolea wito mpinzani wake mkubwa Benny Gantz

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amemtolea wito mpinzani wake mkubwa Benny Gantz waunde serikali ya umoja wa kitaifa.

Katika risala yake kupitia kanda ya video, Netanyahu amesema alipendelea kuunda serikali ya muungano ya mrengo wa kulia lakini matokeo ya uchaguzi yanaonyesha haitowezekana hivyo kumsihi Gantz waunde serikali pana ya umoja.

Bw. Bw.Netanyahu ameongeza kwamba wao kama viongozi wanaowategemea ameomba waunde serikali pana ya umoja kuanzia leo ili kuonyesha kuwa wanawajibika na wanaweza kuendeleaza ushirikiano.

Waziri huyo amesema kwamba hakuna sababu ya kuitisha uchaguzi kwa mara ya tatu, na kwamba suala hilo analipinga hivyo anahitaji serikali pana ya umoja wa kitaifa.

Hata hivyo Bw.Gantz bado hajasema chochote kuhusu wito huo ingawa hapo jana alizungumzia haja ya kuundwa serikali ya umoja, lakini aliondowa uwezekano wa kujumuishwa Benjamin Netanyahu.

Comments

comments

clement

Read Previous

Rais Abdel Fattah al Sissi wa Misri amekutana na waziri mkuu aliyeteuliwa hivi karibuni wa Sudan

Read Next

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!