Netanyahu atoa Wito wa Serikali ya Muungano.

Pendekezo la waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu la serikali ya muungano limekataliwa na aliyekuwa mkuu wa jeshi Benny Gantz.

Moshe Yaalon, kiongozi mkuu wa chama cha Gantz cha Blue and white ametangaza kuwa hawataingia katika muuungano unaoongozwa na Netanyahu badala yake, Gantz ameelezea nia yake ya kuwa waziri mkuu.

Naibu wa Gantz Yair Lapid ametangaza kuwa iwapo Netanyahu atakaa kando basi watabuni serikali ya muungano.

Kwa mujibu wa Vyanzo vya habari nchini humo Netanyahu anakabiliwa na uwezekano wa mashtaka ya ufisadi ambapo Hata hivyo kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 69 ambaye amehudumu kwa muda mrefu zaidi, amekanusha kufanya makosa yoyote.

Rais wa Israel Reuven Rivlin ametangaza kuwa ataanza mashauriano na vyama vyote siku ya Jumapili kuamua anayepaswa kuunda serikali ijayo.

Uchaguzi wa Jumanne kulidhihirisha kwa mara ya kwanza Israel kuandaa uchaguzi mara mbili katika kipindi cha mwaka mmoja. Kura hiyo iliitishwa baada ya chama cha Likud kinachoongozwa na Netanyahu kushindwa kupata kura za kutosha kubuni muungano baada ya uchaguzi wa mwezi Aprili.

Comments

comments

clement

Read Previous

Wajenga kituo cha Afya kwa Milioni 100 waomba nguvu kwa Rais…Wananchi.

Read Next

Serikali yatoa Sh.Bil. Sita kwa miradi ya maendeleo (W) Bunda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!