Wizara yatoa Taarifa kuhusu Ajali ya Ndege Ndogo.

Ofisi ya Kaimu Katibu Mkuu Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, imetoa taarifa fupi kwa vyombo vya habari kuhusu ajali ya ndege ndogo ya kampuni ya AURIC AIR iliyoanguka na kuharibika kabisa majira ya saa moja na nusu leo asubuhi wakati ikianza kuruka kutoka kiwanja kidogo cha SORONERA na kusababisha vifo vya watu wawili.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na naibu katibu mkuu uchukuzi na mhandisi THOMAS NGULIKA, imesema kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea kiwanja cha GRUMETI kwa ajili ya kupakia abiria kabla ya kupata ajali huku taarifa ikieleza kuwa viwanja vyote husika vinamilikiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa TANAPA.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa katika marubani wote wawili waliofariki katika ajali hiyo, ni mmoja tu Nelson Mabeyo ndiye alikuwa na jukumu la kurusha ndege hiyo na rubani mwingine hakuwa na kazi yeyote ndani ya ndege hiyo na haijulikani bado alipanda kwa madhumuni gani.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mkaguzi wa wizara ametumwa kwenda eneo la ajali na anatarajiwa kutoa taarifa rasmi juu ya nini kimesababisha ajali hiyo ambapo wizara imeahidi kutoa taarifa kila hatua ya uchunguzi kwa umma.

Comments

comments

clement

Read Previous

Mazungumzo ya Simu kati ya Trump na Rais wa Ukraine.

Read Next

Wanafunzi 7 wa S/Msingi wapoteza Maisha Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!