Wabunge wa Baraza la Congress nchini Marekani wanataka Trump achunguzwe.

Wabunge wa Baraza la Congress nchini Marekani wameona kuna kila sababu ya kuzingatia malalamiko ya mtu aliyefichua malalamishi dhidi ya Donald Trump yaliyosababisha miito ya kutaka achunguzwe.

Malalamiko hayo yanahusu mawasiliano tata ya simu baina ya Bwana Trump na Rais wa Ukraine vimeeleza vyombo vya habari.

Taarifa za hivi karibuni zinakuja huku kaimu mkurugenzi mkuu wa ujasusi wa Marekani akitarajia kutoa ushahidi juu ya suala hili.

Hata hivyo katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano jioni kwa mara nyingine tena Rais Trump alipuuzilia mbali uchunguzi dhidi yake akiutaja kuwa “feki ” na “wenye hila”.

Ombi hilo la Rais Donald Trump kumtaka Rais wa Ukraine kumsaidia kumchunguza Joe Biden na mtoto wake linaweza kutumika kama chanzo kikubwa cha kumfanyia uchunguzi dhidi yake wenye lengo la kumuondoa madarakani.

Hata hivyo inaelezwa kwamba ombi hilo la Trump kwa Rais Volodymyr Zelenskiy halikuwa la kutaka fedha za kampeni, lakini linatazamwa kama mchango wenye thamani zaidi.

Taarifa alizokuwa akizitafuta Trump za kumchafulia sifa Biden zinaweza kutumika kama silaha dhidi yake wakati wa kampeni kutokana na kwamba huenda akawa mpinzani wake katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

Comments

comments

George Ambangile

Read Previous

Misaada yatolewa kwa Wahanga wa Kojani.

Read Next

Waziri Mkuu asisitiza uadilifu na uaminifu wa Watumishi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram