Riadha Qatar: Fainali Mbio za Mita 800 Wanawake.

Wanariadha Eunice Sum kutoka Kenya na Halimah Nakaayi wa Uganda wamebeba matumaini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye mbio za mita 800 kwa upande wa wanawake, watakaposhiriki hatua ya fainali ya mashindano ya Qatar itakayofanyika leo saa nne usiku katika uwanja Khalifa International.

Nakaayi alifuzu fainali baada ya kushinda nafasi ya kwanza kwenye mchujo uliofanyika Jumamosi, na Eunice akifuzu kwa kushika nafasi ya pili kwenye hatua hiyo.

Mbio za mwaka huu za mita 800 zinatazamwa kuwa hazina mwenyewe kutokana bingwa mtetezi ambaye pia ni tishio, Caster Semenya wa Afrika Kusini kutoshiriki.

Comments

comments

clement

Read Previous

Kansela wa zamani Kurz apata Idadi kubwa ya kura katika uchaguzi wa Bunge.

Read Next

Rais Xi Jinping wa China asisitiza kuwa hakuna nguvu yoyote inayoweza kuizuia China kupiga hatua mbele.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!