Askari 25 wa Mali na wanajihadi 15 wauawa Boulkessi.

Askari wasiopungua 25 pamoja na wanajihadi 15 wamepoteza maisha huku askari wengine zaidi ya 60 wakiwa hawajulikani walipo, baada ya kundi la watu wenye silaha linalodaiwa kuwa na mahusiano na kundi lakigaidi la al-Qaeda kuzishambulia kambi za jeshi zilizoko katikati ya Mali hapo jana.

Taarifa za awali zilizotolewa na msemaji wa kikosi cha wanajeshi kutoka Mali, kilicho chini ya usimamizi wa jeshi la pamoja la G5 Sahel zimesema kikosi hicho kimepoteza askari 25, na askari wengine wakiwa hawajulikani waliko mpaka sasa huku Jeshi hilo pia likipata hasara kubwa ya Vifaa vya kivita vilivyokuwa vimehifadhiwa katika kambi hizo.

Aidha Taarifa hizo zimeendelea kueleza kuwa Mashambulizi hayo yalitokea kwa wakati mmoja kwenye kambi zilizoko Boulikessi na Mondoro ambapo Kwenye kambi ya Boulikessi, washambuliaji hao walikivamia kikosi maalumu cha kulinda usalama katika ukanda wa Sahel.

Msemaji wa serikali ya Mali, Yaya Sangare amesema kundi hilo lilitumia silaha nzito na kusababisha uharibifu mkubwa.Baada ya makabiliano ya risasi, jeshi la Mali lilifanikiwa kurejesha udhibiti wa kambi hiyo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Wabakaji Kalambo kusakwa, agizo la Waziri Lugola.

Read Next

Ziara ya Waziri wa Viwanda, Kiwanda cha Nyuzi .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!