Vikosi vya usalama nchini Iraq vilitumia gesi za kutoa machozi dhidi ya mamia ya waandamanaji

Vikosi vya usalama nchini Iraq vilitumia gesi za kutoa machozi dhidi ya mamia ya waandamanaji waliokuwa wamekusanyika katika eneo la kati mwa Baghdad hii leo, saa chache baada ya amri ya kutotoka nje kutangazwa mjini humo kutokana na siku mbili za ghasia kali ambazo zimeikumba nchi hiyo, huku kukiwa na maandamano dhidi ya serikali.

Inaelezwa kwamba kulisikika milipuko usiku wa manane ndani ya eneo lililo na ulinzi mkali la Green Zone mjini Baghdad ambako ni eneo la ofisi za serikali na balozi za mataifa ya kigeni.

Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani umesema uchunguzi unaendelezwa na kuongeza kuwa hakuna mali ya vikosi hivyo vya muungano iliyolengwa.

Kufikia sasa takriban watu tisa wameripotiwa kupoteza maisha na mamia wamejeruhiwa tangu ghasia zilipozuka siku ya Jumanne wiki hii kati ya vikosi vya usalama vya serikali na waandamanaji wanaoipinga serikali .

Comments

comments

clement

Read Previous

Serikali imesema haitasita kuzifutia leseni kampuni zinazohusika na uuzaji wa mbolea

Read Next

Wahandisi wa Maji wapewa changamoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!