China yatakiwa kumchunguza Joe Biden.

Rais wa Marekani Donald Trump ameitaka China imchunguze aliyekuwa makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden licha ya Rais huyo kukabiliwa na kitisho cha kufanyiwa uchunguzi unaoweza kusababisha aondolewe madarakani.

Uchunguzi huo dhidi ya Trump unatokana na madai kwamba alimshinikiza Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amchunguze Bw. Biden na mwanawe Hunter Biden.

Trump aliwaambia waandishi wa habari ikulu, kwamba China inapaswa kuanza uchunguzi huo hata hivyo ameeleza kwamba hakumuomba Rais wa China Xi Jinping moja kwa moja lakini anafikiria kufanya hivyo.

Mwenyekiti wa kamati ya upelelezi ya bunge la Marekani Adam Schiff amesema kauli zaTrump zinaonyesha Rais huyo anahisi kuwa anaweza kufanya anachotaka bila ya kuwajibishwa.

Comments

comments

clement

Read Previous

Msaada wa Kiasi cha Euro Milioni 1 kutoka Ujerumani.

Read Next

Ziara ya Rais Dkt. Magufuli Mkoani Rukwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!