Msaada wa Kiasi cha Euro Milioni 1 kutoka Ujerumani.

Serikali ya Ujerumani imekubali kutoa kiasi cha Euro milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa mfumo wa kutambua mapema virusi vinavyosababisha homa ya Ebola.

Waziri wa Afya wa Ujerumani Jens Spahn amesema hayo kwenye mkutano wa wafadhili ulioandaliwa na Umoja wa Afrika mjini Adis Ababa.

Fedha hizo pia zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya udhibiti na kuepusha maambukizi yanayotokea katika nchi kadhaa za Afrika.

Waziri wa Afya wa Ujerumani amesisitita umuhimu wa vituo hivyo katika juhudi za kuepusha maambukizi ya Ebola alipokutana na kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia masuala uhamiaji na afya Amira El Fadil.

Comments

comments

clement

Read Previous

Lugola awachukulia hatua viongozi wa Polisi watatu Nkasi.

Read Next

China yatakiwa kumchunguza Joe Biden.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!