Mtu mmoja amefariki Dunia na wengine 30 wamejeruhiwa kufuatia Ajali ya Barabarani.

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 30 wamejeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha magari tatu kugongana katika eneo la kasanga manispaa ya Morogoro na katika majeruhi hao 14 ni wanaume na 16 wanawake .

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Issack Katamiti amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni baada ya dereva wa basi la abiria lenye namba za usajili T801 DBF kutaka kulipita roli lililokuwa mbele yake na kugongana uso kwa uso na Fuso lililokuwa likitoka maeneo ya mikumi kuelekea Morogoro na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye ni Dereva wa Roli .

Dkt.Ritha Lyamuya ni mganga mfawidhi hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro amesema kuwa kati ya majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo tayari 21 wamepatiwa matibabu na wengine tisa waliobaki wanaendelea na matibabu huku wagonjwa wawili kati yao wakipatiwa rufaa ya kuenda hospitali ya taifa mhimbili

Comments

comments

clement

Read Previous

Wanafunzi zaidi ya 300 wasimamishwa Shule, Mbeya.

Read Next

Lugola awachukulia hatua viongozi wa Polisi watatu Nkasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!