Watu 100 wauawa katika Maandamano Nchini Iraq.

Takriban watu 100 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 400 kujeruhiwa , katika maandamano ya kupinga serikali nchini Iraq kutokana na na makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama.

Maandamano dhidi ya serikali nchini humo yaliingia siku ya tano hapo jana katika mji mkuu Baghdad na majimbo mengine huku waandamanaji wakichoma moto ofisi za umma na kupuuza miito ya utulivu kutoka viongozi wa kisiasa na dini.

Tangu siku ya Jumanne, maelfu ya watu wameingia barabarani nchini humo na kuandamana kupinga rushwa, ukosefu wa ajira, maji safi na huduma mbovu hasa za umeme.

Hapo jana viongozi wa kisiasa walishindwa kuitisha kikao cha dharura cha bunge kujadili matakwa ya waandamanji, baada ya kiongozi wa walio wengi bungeni Muqtada al-Sadr kuamuru kikao hicho kisusiwe.

Siku ya Ijumaa Al-Sadr alitoa wito wa kujiuzulu kwa serikali ya waziri mkuu Abdul-Mahdi na kuitishwa uchaguzi wa mapema akisema umwagaji damu wa raia haupaswi kupuuzwa.

Maandamano ya Iraq ambayo kwa kiasi kikubwa yanaongozwa na vijana yaliibuka tena mwishoni mwa wiki baada ya amri ya kutotoka nje kuondolewa mjini Baghdad, mapema siku ya Jumamosi.

Comments

comments

clement

Read Previous

Ziara ya Rais Dkt. Magufuli Mkoani Rukwa.

Read Next

Zaidi ya Watu 20 wauawa kwa Shambulio la mgodi nchini Burkina Faso.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!