Agizo : Wanaowapa watoto mimba wakamatwe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli ameviagiza vyombo vya dola pamoja na viongozi wa Mkoa wa Rukwa kuwachukulia hatua kali kwa kuwapeleka mahakamani watu ambao wamekuwa wakikwamisha ndoto za watoto wa kike ambao bado wanasoma kwa kuwapa mimba.

Mhe. Rais ametoa agizo hilo kwa uongozi wa wilaya na mkoa pamoja na karipio dhidi ya watu wanaositisha ndoto za watoto wa kike kupata haki yao ya msingi ya elimu alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini Sumbawanga akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani humo ambapo ameelezea kusikitishwa kwake na idadi kubwa ya watoto waliopata mimba mwaka jana ambayo ilifikia jumla ya wanafunzi 229 hali ambayo amesema inasikitisha.

Ameelezea kushangazwa na hali hiyo ambapo ametumia fursa hiyo kuuagiza uongozi wa Wilaya na Mkoa pamoja na vyombo vya dola kuwakamata wahusika waliowapa mimba wanafunzi hali ambayo amesema ina athiri juhudi za serikali inayotumia fedha nyingi kutoa elimu bila malipo ili watoto wote wasome.

Wakati huo huo Mhe. Rais Magufuli amewasisitizia watendaji wa Serikali kuanzia ngazi za chini hadi za juu kuwa na weledi pamoja na kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ile jamii.

Aidha Mhe. Rais Magufuli amesema kuwa Miradi ya Maji, Barabara, pamoja na mingine itaendelea kuboreshwa na serikali ili wananchi waendelee kupata huduma bora pamoja waweze kushiriki kazi ya kukuza uchumi wao akitoa mfano kwa mkoa wa Rukwa kujikita katika Kilimo ambao umekuwa mkoa wa pili kitaifa katika kilimo.

Awali Mhe. Rais Magufuli alifungua Msikiti wa Itiqaama Bomani uliopo Sumbawanga Mjini na kuwahimiza watanzania kutumia nyumba za ibada kuimarisha upendo, amani na mshikamano miongoni mwao, kama inavyosisitizwa na maandiko matakatifu ya dini zote. Rais alichangia shilingi milioni 5 kwa ajili ya msikitiki huo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Vigogo wa CHADEMA, Njombe wahamia CCM

Read Next

Ennahda kinaongoza matokeo ya awali Uchaguzi Tunisia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!