Ennahda kinaongoza matokeo ya awali Uchaguzi Tunisia.

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa bunge nchini Tunisia yanaonesha kuwa chama cha Kiislamu chenye msimamo wa wastani, Ennahda kinaweza kuibuka na ushindi katika bunge lijalo.

Muda mfupi baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa jana jioni, chama cha Ennahda na chama cha kiliberali cha Heart of Tunisia vilijitangazia ushindi.

Tume ya uchaguzi ya Tunisia imesema asilimia 41 ya watu walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi huru wa tatu wa bunge tangu kutokea kwa vuguvugu la mapinduzi mwaka 2011 lililouondoa madarakani utawala wa kimabavu na kuanzisha demokrasia pamoja na kuanza kutumika kwa katiba mpya 2014.

Comments

comments

clement

Read Previous

Agizo : Wanaowapa watoto mimba wakamatwe.

Read Next

Trump, Erdogan wazungumzia eneo salama Mto Euphrates.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram