Trump, Erdogan wazungumzia eneo salama Mto Euphrates.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mwenzake wa Marekani Donald Trump wamejadiliana kuhusu uwepo wa eneo salama mashariki mwa Mto Euphrates.

Wakizungumza jana kwa njia ya simu, Erdogan amerudia kusisitiza msimamo wake wa kuanzishwa eneo salama hatua itakayotuliza kitisho kinacholetwa na Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi, PKK na kundi la wanamgambo wa Kikurdi, YPG linaoungwa mkono na Marekani.

Ofisi ya Erdogan imebainisha kuwa hatua hiyo itasaidia kuanzisha mazingira muhimu ya kurejea kwa wakimbizi wa Syria.

Erdogan pia amemueleza Trump masikitiko yake kutokana na majeshi ya Marekani na urasimu wa usalama kushindwa kutekeleza makubaliano kati ya nchi hizo mbili.

Viongozi hao wawili wamekubaliana kukutana mjini Washington mwezi ujao kufuatia mwaliko wa Trump.

Comments

comments

clement

Read Previous

Ennahda kinaongoza matokeo ya awali Uchaguzi Tunisia.

Read Next

Wakazi wa DSM wajitokeza kwa wingi zoezi la uandikishaji daftari la mpiga kura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!