Vigogo wa CHADEMA, Njombe wahamia CCM

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Njombe kimepata pigo kwa viongozi wake wa ngazi ya juu kuendelea kukihama, baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wake wa mkoa wa Njombe, Wakili Edwin Swale kutangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichoeleza hana sababu ya kumpinga Rais Dk. John Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa kama kambi ya upinzani na badala yake ametoa wito Rais aungwe mkono kuendelea na kasi ya maendeleo nchini.

Hayo ameyasema aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Njombe Edwin Swale ambaye pia ni Wakili msomi aliyeamua kukabidhi rasmi kadi ya uanachama wa Chadema kwa mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Njombe, Edward Mgaya na kubainisha kile kilichomsukuma kujiunga na CCM akitoke upinzani akiwa ameongoza na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bavicha Tarafa ya Lupembe Msafiri Mpolo

Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ya Njombe, Edward Mgaya ametumia wasaa wa kuwapokea wanachama hao wapya kutoka Chadema kwa kuwataka kwenda kuunganisha nguvu na mbunge wa Jimbo la Lupembe, Jorum Hongoli kwa lengo la kukuza uchumi kwa wananchi wa Tarafa ya Lupembe kupitia kilimo mbalimbali

Comments

comments

clement

Read Previous

Wakulima, Wafugaji pamoja na Wavuvi, kisiwani Pemba wametakiwa kufuata taarifa za wataalamu za Hali ya Hewa

Read Next

Agizo : Wanaowapa watoto mimba wakamatwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!