Waathiriwa Utawala wa Dikteta Yahya Jammeh walipwa fidia.

Serikali ya Gambia imetoa euro 900,000 kwa mfuko wa misaada wa waathiriwa wa utawala wa Dikteta Yahya Jammeh ikiwa ni pesa zilizotokana na mali ya kiongozi huyo wa zamani wa Gambia, baada ya kukamatwa na serikali na kuuzwa.

Uuzaji wa mali za Yahya Jammeh unatajwa utaleta manufaa makubwa kwa Gambia. Kiongozi huyo alikuwa na mali zaidi ya 280, ikiwa ni pamoja na biashara na hifadhi za misitu na visiwa huku pia akishutumiwa kupitisha kwa mlango wa nyuma karibu dola milioni 360 kutoka hazina ya serikali.

Waziri wa Sheria nchini Gambia Abubacarr Tambadou, amekaribisha hatua ya serikali ya kuwapa waathiriwa fedha zilizoibwa na Dikteta Jammeh na kusema kuwa Serikali inaamini kuwa kutumia utajiri na mali za mtawala huto wa zamani kwa kulipa fidia waathirika wa utawala wake ndio njia bora na nzuri zaidi.

Sheriff Kijera ambaye ni kiongozi wa kituo cha kinachohudumia waathiriwa amesema serikali kwa kukabidhi mali hizo ni mpango wenye ishara nzuri ingawa fedha hizo hazitoshi kulipa fidia kwa waathiriwa wote.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Wakazi wa DSM wajitokeza kwa wingi zoezi la uandikishaji daftari la mpiga kura.

Read Next

Korea Kaskazini yaonya iwapo kutazushwa mjadala wa Nyuklia kwenye UN.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!