Korea Kaskazini yaonya iwapo kutazushwa mjadala wa Nyuklia kwenye UN.

Korea Kaskazini imezionya nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kwamba iwapo wataliibua suala la majaribio yake ya makombora kwenye mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa inawezekana hatua hiyo ikaongeza zaidi nia yake ya kulinda uhuru wa taifa hilo.

Mataifa 15 wanachama wa baraza hilo wanatarajiwa kukutana katika kikao cha ndani kufuatia ombi la nchi za Ujerumani, Uingereza na Ufaransa baada ya Korea Kaskazini wiki iliyopita kufyatua kombora jipya linaloweza kurushwa kutokea kwenye nyambizi.

Balozi wa Korea Kaskazini katika Umoja huo Kim Song alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na namna watakavyoulinda uhuru wa taifa hilo aliwajibu waandishi hao waendelee kufuatilia kwa makini kuona kile watakachokifanya huko mbeleni na kuongeza kuwa hiyo haimaanishi watafyatua kombora jingine.

Pyongyang inatoa onyo hilo ikiamini kwamba Marekani iko nyuma ya vuguvugu hilo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Waathiriwa Utawala wa Dikteta Yahya Jammeh walipwa fidia.

Read Next

Uzinduzi wa Barabara ya Kanazi – Kizi – Kibaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram