Wakazi wa DSM wajitokeza kwa wingi zoezi la uandikishaji daftari la mpiga kura.

Siku ya kwanza kuanza kwa zoezi la kujiandikisha katika daftari la mpiga kura baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salam wamejitokeza kutumia fursa hiyo ambayo itawaruhusu kuchagua kiongozi wanaemtaka na kuwataka wengine kujitokeza badala ya kusubiri siku za mwisho.

Wakizungumza na channel ten wakazi hao wamesema wapo baadhi ya watu wanaogopa kwenda kujiandikisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokujua kuandika jambo ambalo haliathiri zoezi hilo na kwamba ni vema watanzania wakaondoa itikadi za kisiasa wakati huu wa kujiandikisha ili kuepuka mgongano unaoweza kujitokeza.

Baadhi ya mawakala waliozungumza na channel Ten wamesema zoezi linaenda vizuri lakini wakaomba serikali kutangaza zaidi hata kwa kutumia magari ya matangazo ili wananchi wengi wajitokeze kutumia fursa hii ndani ya siku zilizopangwa kuanzia oktoba 8 hadi 14.

Comments

comments

clement

Read Previous

Trump, Erdogan wazungumzia eneo salama Mto Euphrates.

Read Next

Waathiriwa Utawala wa Dikteta Yahya Jammeh walipwa fidia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!