Dar Es Salaam yabuni mpango wa kupokea malalamiko.

Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda amezindua Mfumo wa kuratibu Malalamiko ya wananchi na Uwajibikaji wa watendaji kuanzia ngazi ya Mtaa, kata hadi wilaya Mfumo ambao wananchi watatoa malalamiko yako kupitia Mfumo wa Technolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA ambao Mkuu wa Mkoa atapata Malalamiko hayo moja kwa moja.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mfumo huo Makonda amesema Mwananchi atakuwa na Uwezo wa kueleleza kero,Usumbufu au kutowajibika kwa kiongozi wa eneo husika na kuwataka wananchi kuutumia Mfumo huo kwa nia njema ili kuendelea uwajibikaji kwa viongozi waliopewa dhamana ya kuwahudumia wananchi.

Aidha Makonda Pia alitumia fursa hiyo kuendelea kuwasihi wananchi wa Mkoa wa Dsm hususan wanaoishi kando ya Mito au Mabondeni kuchukua tahadhari kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha.

Comments

comments

clement

Read Previous

Waziri Mkuu asisitiza Mshikamano kwa Watanzania.

Read Next

Waliovamia eneo watakiwa kuondoka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!