Makamu wa Rais ajiandikisha Daftari la Wapiga Kura.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha katika daftari la wapiga kura kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ili utakapofika wakati wa uchaguzi wachague viongozi waadilifu.

Mama Samia ametoa wito huo jijini Dodoma alipojitokeza kujiandikisha katika kituo cha kupiga kura cha Kilimani kilichopo mtaa wa Salmini katika kata ya Tambukareli ikiwa ni siku ya pili tangu kuanza kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura nchi nzima.

Mkoa wa Dodoma unalenga hadi zoezi la uandikishaji litakapokamilika ndani ya siku saba wapiga kura zaidi ya laki 9 wawe wamejiandikisha kwenye vituo zaidi ya elfu tatu.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge anasema makadirio hayo yanaweza yakavukwa kwani kwa siku ya kwanza pekee ya uandikishaji watu zaidi ya laki moja na nusu wamejitokeza, huku baadhi ya wananchi waliojiandikisha wakitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili washiriki kuchagua viongozi katika uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.

Comments

comments

clement

Read Previous

Uzinduzi wa Barabara ya Kanazi – Kizi – Kibaoni.

Read Next

Serikali ya Trump yakataa kutoa ushirikiano wa Kumshtaki Rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!