Serikali ya Trump yakataa kutoa ushirikiano wa Kumshtaki Rais.

Ikulu ya Marekani imesema Serikali ya Rais Donald Trump haitatoa ushirikiano katika kile inachokiita uchunguzi usio halali wa kumshitaki Rais uliopendekezwa na chama cha Democratic.

Katika barua iliyotumwa kwa Viongozi wa Bunge hilo, mawakili wa Serikali ya Trump wameeleza wazi kwamba hawatoshiriki hatua ambayo inaonesha kuwa Trump sasa anaweza kuingia katika mvutano wa kikatiba na bunge.

White House imesisitiza kwamba Bunge halikupiga kura rasmi ya kuanza uchunguzi huo, na kuongeza kuwa kutokana na hilo linakosa mamlaka kamili ya kufanya mchakato wa kumshitaki Trump.

Akijibu barua hiyo Spika wa Bunge Nancy Pelosi amesisitiza kwamba bunge lina haki ya kikatiba ya kuzifuatilia taasisi za juu bila ya kuzingatia kura rasmi ya mchakato huo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Makamu wa Rais ajiandikisha Daftari la Wapiga Kura.

Read Next

Waziri Mkuu asisitiza Mshikamano kwa Watanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!