Uzinduzi wa Barabara ya Kanazi – Kizi – Kibaoni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wa ngazi zote na watendaji wa chama na Serikali kuzungumzia mafanikio ya utekelezaji wa miradi mikubwa inayogusa wananchi ambayo inatekelezwa na Serikali katika maeneo yao.

Mhe.Rais.Magufuli ametoa wito huo katika eneo la kibaoni wilayani Mlele mkoani Katavi wakati alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye hafla ya uzinduzi wa barabara ya Kanazi – Kizi – Kibaoni yenye urefu wa Kilomita 76.7 ambayo imejengwa kwa gharama ya Shs Bilioni 100.5, fedha iliyotolewa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100.

Mhe.Rais Magufuli amesisitiza kwamba lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuwahudumia wananchi kwa kuwatatulia kero zao ambapo amewakumbusha viongozi na watendaji kuhusu umuhimu wa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Katika hatua nyingine, Mhe.Rais Magufuli amezungumzia migogoro ya ardhi katika eneo hilo ambalo ni la wakulima na wafugaji ambapo amewataka wananchi kuchapa kazi.

Nao Mawaziri waliofutana na Mhe. Rais katika ziara hiyo wakaeleza utekelezaji wa miradi na majukumu kupitia Wizara wanazoziongoza.

Comments

comments

clement

Read Previous

Korea Kaskazini yaonya iwapo kutazushwa mjadala wa Nyuklia kwenye UN.

Read Next

Makamu wa Rais ajiandikisha Daftari la Wapiga Kura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!