Waziri Mkuu asisitiza Mshikamano kwa Watanzania.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kushikamana na wazingatie ujumbe wa mbio za mwenge za mwaka huu unaohimiza umuhimu wa maji, uchaguzi wa Serikali za mitaa, vita dhidi ya rushwa, malaria, UKIMWI na dawa za kulevya.

Akizungumza na viongozi wa Halmashauri za Lindi na Ruangwa pamoja na wananchi wa kijiji cha Nangumbu katika uwanja wa shule ya msingi Nangumbu ambako mwenge huo ulipokelewa saa 1:44 asubuhi ukitokea Nyangao wilayani Lindi, Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa, pia amewahimiza wananchi wote wajiandikishe kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili Tanzania iweze kupata viongozi bora.

Waziri Mkuu yupo wilayani Ruangwa ili kushiriki mbio za mwenge wa uhuru, ambapo kesho mwenge huo utaelekea Nachingwea, Ijumaa utakwenda Liwale, Jumamosi Kilwa na Jumapili utakuwa Manispaa ya Lindi ambako utahitimisha mbio zake na kuzimwa Jumatatu Oktoba 14, mwaka huu.

Mapema, akizungumza baada ya kupokea mwenge huo saa 2:21 asubuhi, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa alisema utakimbizwa kwenye kata saba na vijiji 17 ambapo miradi mitatu mikubwa yenye thamani ya sh. bilioni 2.9 itazinduliwa, ambapo Ukiwa njiani, mwenge huo ulipitishwa kijiji cha Nandagala ambako Waziri Mkuu alizaliwa, aliupokea na kuukimbiza kidogo akiwa na wanakijiji wenzake.

Akizungumza kabla ya kuanza kwa mbio za mwenge wilayani Ruangwa, kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa, Bw. Mzee Ali Mkongea
alisema Serikali ya awamu ya tano, ndani ya miaka mitatu imekamilisha kwa wakati miradi 124 ya maji, baadhi yake ikiwa ni miradi mikubwa ya Chalinze, Bagamoyo, Arusha, Tabora na Musoma.

Comments

comments

clement

Read Previous

Serikali ya Trump yakataa kutoa ushirikiano wa Kumshtaki Rais.

Read Next

Dar Es Salaam yabuni mpango wa kupokea malalamiko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!