Waliovamia eneo watakiwa kuondoka.

Mkuu wa Wilaya ya Wete Kapteni Khatib Khamis Mwadini amewataka wananchi waliovamia eneo lililotengwa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa mji mpya huko Finya kuvunja nyumba zao kwani hakuna atakayelipwa fidia wakati ujenzi utakapoanza.

Agizo hilo amelitoa wakati akizungumza katika kikao cha kujadili mpango wa Uendelezaji wa Mji wa kisasa wa Finya kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa baraza la mji Wete.

Amesema uwepo wa mji wa kisasa ni jambo linalovutia wengi hivyo ni vyema wananchi watakaopewa viwanja kuviendeleza kama ilivyokusudiwa, huku Katibu Tawala Mkoa wa Kaskazini Pemba Bakar Ali Bakar akitoa angalizo wakati wa ugawaji wa viwanja..

Afisa Mdhamini wizara ya Ardhi, Nyumba , Maji na Nishati Pemba , Juma Bakar Alawi amewataka wananchi kuzitumiaa taasisi husika kuwasilisha maombi ya viwanja huku Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete Hamad Mbwana Shehe ameahidi kusimamia kutekeleza mpango huo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Dar Es Salaam yabuni mpango wa kupokea malalamiko.

Read Next

Jeshi la Polisi Tarime RORYA lawashikilia watano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!