Meli ya Mafuta ya Iran yashambuliwa Saudia.

Makombora mawili yameipiga meli ya mafuta ya Iran katika Bahari ya Shamu kwenye Pwani ya Saudi Arabia, ikiwa ni tukio la karibuni katika jimbo hilo kufuatia miezi kadhaa ya mivutano kati ya Iran na Marekani.

Televisheni ya taifa ya Iran imesema mlipuko huo uliharibu vyumba viwili vya meli hiyo na kusababisha kuvuja kwa mafuta katika Bahari ya Shamu karibu na mji wa bandari wa Saudia wa Jiddah. Saudi Arabia haijatoa taarifa yoyote kuhusu madai ya shambulizi hilo.

Jeshi la wanamaji la Marekani linaloendesha operesheni zake Mashariki ya Kati limesema maafisa wamefahamishwa kuhusu ripoti za tukio hilo, lakini wakakataa kutoa taarifa zaidi.

Tukio hilo limetokea baada ya Marekani kudai katika miezi ya nyuma kuwa Iran ilizishambulia meli za mafuta karibu na Mlango wa bahari wa Hormuz, katika Ghuba ya Uajemi kitu ambacho Iran ilikanusha.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Rushwa kumfikisha Zuma Mahakamani.

Read Next

Rais aviagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama Katavi kuwa Imara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!