Mkuu wa Mkoa awatembelea Wahanga wa Mafuriko Korogwe.

Mkuu wa Mkoa Tanga MARTINE SHIGELA amewatembelea na kuwapa pole wahanga walioathirika na mafuriko ya Mvua zilizosababisha vifo vya watu tisa mpaka sasa katika Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga pamoja na kutoa kilo zaidi ya mia sita za mchele kwa wahanga hao.

Akizungumza na Wananchi hao Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa atazungumza na wawekezaji wa Mashamba ambayo hawayafanyii kazi ili kuwapatia wananchi baadhi ya maeneo kwaajili ya Makazi yaliyo imara pamoja na shughuli za kilimo.

Kwa upande wao Wabunge wakaelezea adha iliyowakuta wananchi wao huku wakiwataka kuwa wasikivu katika kipindi hiki.

Aidha Mkuu wa Mkoa pia akawataka Tarura pamoja na Tanroads kufanyia kazi miundombinu yao yenye changamoto zilizoleta mafuriko hayo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Onyo la CCM kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Read Next

Waziri Mkuu Ethiopia ashinda Tuzo ya Nobel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!