Waziri Mkuu Ethiopia ashinda Tuzo ya Nobel.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameshinda Tuzo ya Amani ya Nobel 2019 kutokana na juhudi zake muhimu za kuutatua mzozo wa mpakani na nchi jirani ya Eritrea.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nobel nchini Norway Berit Reiss-Andersen amesema Abiy mwenye umri wa miaka 43, alichaguliwa kutokana na juhudi zake za kuleta amani na ushirikiano wa kimataifa.

Kabla ya hapo majina kadhaa yalitajwa ikiwa ni pamoja na mwanaharakati wa kupigania usafi wa mazingira, raia wa Sweden, Greta Thunberg mwenye umri wa miaka 16, waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na wanaharakati wanaopigania mageuzi Hong Kong.

Idadi ya walioshindania tuzo ya mwaka huu ilijumuisha watu 223 na mashirika 78.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Mkuu wa Mkoa awatembelea Wahanga wa Mafuriko Korogwe.

Read Next

Rushwa kumfikisha Zuma Mahakamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!