Kenya yavunja rekodi iliyowekwa miaka 16 iliyopita.

Mwanadada Brigid Kosgei wa Kenya amevunja rekodi ya mbio za Marathon Wanawake iliyodumu kwa miaka 16 kwa kukimbia muda mfupi zaidi kwenye umbali wa kilomita 42.

Brigid alitumia Saa 2 Dakika 14 na Sekunde 4, kwenye mbio za Chicago Marathon zilizofanyika jana, na kuipiku rekodi iliyowekwa na mwingereza Paula Radcliffe mwaka 2003 alipotumia Saa 2 Dakika 15 na Sekunde 25.

Wadau mbalimbali wa michezo pamoja na watu mashuhuri wamempongeza mfukuza upepo huyo kwa kuifikia rekodi hiyo ambayo imewahi kuwa rekodi ya kukimbia umbali huo kwa wanaume, akiwemo Rais wa zamani wa marekani Barack Obama.

Katika mbio hizo za chicago nafasi ya pili na nafasi ya tatu zilitwaliwa na wanariadha wawili kutoka Ethiopia, Ababel Yeshaneh na Gelete Burka mtawalia.

Comments

comments

clement

Read Previous

Polisi Nchini Kenya yaimarisha Usalama Kaunti ya Mandera.

Read Next

Matokeo Mitihani ya Darasa la Saba yatangazwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!