Polisi Nchini Kenya yaimarisha Usalama Kaunti ya Mandera.

Polisi katika Kaunti ya Mandera, Kaskazini Mashariki mwa Kenya wapo katika hali ya tahadhari, baada ya kuripotiwa kuwa washukiwa 20 wa Al Shabab kutoka nchini Somalia wameonekana katika eneo hilo.

Ripoti zinasema kuwa, magaidi hao walionekana katika maeneo ya Bale-Ilman Mala na Kutulo Ijumaa ya wiki iliyopita.

Haya yanajiri wakati huu miili ya maafisa 11 wa polisi waliouawa Jumamosi iliyopita huko Garissa wakati gari lao lilipokanyaga kilipuzi kilichotegwa ardhini ikirejeshwa jijini Nairobi.

Kenya imeendelea kuwa kwenye vita na kundi la Al Shabab tangu mwaka 2011, ilipotuma wanajeshi wake nchini humo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Kilele cha Mbio za Mwenge na Miaka 20 Bila Baba wa Taifa.

Read Next

Kenya yavunja rekodi iliyowekwa miaka 16 iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!