Matokeo ya Uchaguzi Nchini Msumbiji.

Matokeo yasiyo rasmi ya uchaguzi wa Rais nchini Msumbiji, yanaonesha kuwa chama cha Rais Felipe Nyusi cha FRELIMO, kinaelekea kushinda.

Matokeo yanayoonyesha muelekeo huo yametolewa na taasisi ya kiraia ya Saa-da-paz ya nchini humo.

Wachambuzi wa siasa kufuatia mwelekeo huo wametahadharisha kufanyika kwa udanganyifu wa matokeo, hali ambayo itasababisha usalama wa nchi hiyo kuendelea kuyumba.

Tume ya uchaguzi ya Msumbiji bado haijatoa matokeo rasmi lakini taasisi ya kiraia ya Saa-da-Paz imesema inatazamia kuwa Rais Nyusi amepata ushindi wa asilimia 71 ya kura na kumuacha mbali kiongozi wa chama cha Upinzani cha RENAMO, Ossufo Momade mwenye asilimia 21 ya kura. Iwapo RENAMO itayapinga matokeo, itakuwa pigo kubwa kwa juhudi za amani nchini Msumbiji.

Chama cha RENAMO na serikali walitia saini makubaliano ya amani mwezi Agosti lakini waasi wapatao 5,800 wenye silaha wafuasi wa chama cha Renamo bado hawajarudisha silaha zao.

Comments

comments

clement

Read Previous

Waziri Mkuu wa Uingereza kuwasilisha Makubaliano Mapya ya Brexit Bungeni.

Read Next

Sarfaraz avuliwa unahodha wa Timu ya Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!