Riek Machar atahadharisha Nchi yake kurejea kwenye Vita.

Kiongozi wa upinzaji nchini Sudan Kusini Riek Machar ametaka mchakato wa kuundwa serikali ya muungano uongezwe muda hadi mwisho wa mwezi Desemba mwaka huu.

Machar ametahadharisha uwezekano wa nchi hiyo kurudi kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ikiwa serikali hiyo ya muungano itaundwa ndani ya muda uliowekwa sasa wa tarehe 12 Novemba.

Machar alitoa pendekezo hilo kwa ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliokutana naye pamoja na Rais Salva Kiir kwa ajili ya kusisitiza utekelezaji wa hatua za kuiondoa Sudan Kusini kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe, vya miaka mitano.

Baraza hilo limesikitishwa na kauli ya Riek Machar kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyopo kwa mwaka mmoja sasa yanaweza kuvunjika.

Comments

comments

clement

Read Previous

Kuchelewa kwa Ujenzi wa Lami Matai

Read Next

Chile yaongeza hali ya hatari huku idadi ya Vifo ikiongezeka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!