Hatma ya ombi la Uingereza kuhusu Brexit kujulikana.

Mabalozi kutoka Mataifa ya Umoja wa Ulaya wanakutana leo, kujadili hatma ya Uingereza katika Umoja huo na kuamua nchi hiyo iongezewe muda gani, ili wabunge wapitishe mapendekezo mapya ya kujiondoa kwenye umoja huo.

Ripoti zinasema kuwa, baadhi ya mabalozi hao wanataka Uingereza ipewe muda wa miezi mitatu.

Tayari Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema kuwa, iwapo wataongezewa muda hadi mwezi Januari mwaka 2020, ataitisha Uchaguzi Mkuu wa mapema huku akiendelea kusisitiza kuwa anataka Uingereza iondoke kwenye Umoja huo ifikapo tarehe 31 mwezi huu.

Bwana Johnson amesema uchaguzi unaweza ukahitajika kama njia ya kuondoa mkwamo wa Brexit, lakini chama cha Upinzani cha Labour kimetaka kujadiliwa kwanza kwa tarehe hiyo ya mwisho ya Brexit ambayo ni Oktoba 31.

Comments

comments

clement

Read Previous

Kongomano lajadili athari za Vikwazo dhidi ya Zimbabwe.

Read Next

Nchi za SADC zatakiwa kulinda mazingira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!