Machafuko yaongezeka Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Machafuko yanaendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, licha ya mkataba wa amani uliotiwa saini hivi karibuni kati ya makundi 14 yenye silaha na serikali.

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) imelaani mwenendo wa kundi la UPC kwa kukiuka kanuni za mkataba wa amani ambao ilitia saini.

Minusca imeorodhesha visa kati ya 50 na 70 vya ukiukaji wa mkataba wa amani kila wiki. Machafuko hayo yanahusisha makundi mawili, MLCJ na FPRC, ambayo yalitokea katika mkoa wa Birao Kaskazini mashariki mwa nchi, ambapo watu takriban 24,000 walilazimika kuyatoroka makaazi yao.

Hivi karibuni kikosi cha Umoja wa Mataifa kilifanya operesheni dhidi ya kundi la 3R katika eneo la Karoui, Kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Wakati huo huo kundi jingine la UPC limeendelea kutuma wapiganaji wake Kusini Mashariki mwa nchi hiyo huku raia wakiendelea kuwa na wasiwasi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo licha ya makundi hayo na serikali kutia saini kwenye mkataba wa amani.

Comments

comments

clement

Read Previous

Serikali yaonya Kampeni za Uchaguzi kabla ya wakati.

Read Next

Viongozi wa TAMA AMCOS watoweka na Shilingi Milioni 21.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!