Trump atangaza kuuawa kwa kiongozi wa IS Abu Bakr-Al-Baghdadi Syria.

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza Kiongozi wa Kundi la Dola la Kiislamu Abu Bakr Al-Baghdadi amejiuwa kwa kujilipua na mabomu aliyojifunga mwilini baada ya kikosi maalumu cha Marekani kumnasa katika eneo la ujia wa mwisho wa andaki nchini Syria.

Akizungumza kutoka Ikulu ya White House, Trump amesema Abu Bakr al-Baghdadi alijilipua yeye pamoja na watoto wake watatu wakati alipobaini kuzingirwa na kikosi maalum cha Marekani katika eneo la mwisho wa andaki nchini Syria na kuongeza kuwa mwili wake ulivurugika kwa mlipuko lakini vipimo vya DNA vilitoa matokeo yasiyo na shaka kuwa ni yeye.

Baghdadi alipata umaarufu mwaka 2014, alipotangaza kubuniwa kwa “Himaya ya Kiislamu” katika maeoneo Iraq na Syria ambapo wapiganaji hao walianzisha utawala wa kikatili dhidi ya watu wapatao milioni nane katika maeneo waliyokuwa wanayashikilia.

Kundi hilo pia linalaumiwa kwa kufanya mashambulizi kadhaa katika miji mbalimabli duniani pamoja na udhalimu na maovu yaliyosababisha vifo vya maelfu ya watu.

Comments

comments

clement

Read Previous

Rais Dkt. Magufuli apokea hati za Utambulisho za Mabalozi.

Read Next

Waliofariki kwenye Ajali Handeni watambuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!