Mafuriko Nchini Somalia, Watu 182,000 wakosa Makazi.

Umoja wa Mataifa umesema mafuriko makubwa yamesababisha watu 182,000 nchini Somalia kulazimika kuyahama makazi yao.

Ofisi ya Mratibu wa shirika la misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa katika taarifa yake imesema kumekuwa na uharibifu mkubwa wa miundombinu, mashamba na kufurika kwa mito.

Japo idadi kamili ya waliopoteza maisha katika mafuriko hayo haijajulikana, mmoja wa wa wafanyakazi wa vikosi vya uokoaji kutoka shirika la msalaba mwekundu lililopo katika mji mkuu Mogadishu amesema wamepata miili mitano ya watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko hayo.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Maporomoko ya Matope Cameroon yaua 42.

Read Next

Idadi ya Vifo kutokana na Tetemeko la Ardhi Ufilipino yafikia Saba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!