Maporomoko ya Matope Cameroon yaua 42.

Nchi ya Cameroon imekumbwa na maporomoko ya matope magharibi mwa nchi hiyo yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini humo, Inaaminika bado kuna watu wengine kadhaa wamekwama chini ya maporomoko hayo, huku operesheni za uokoaji zikiendelea katika mji wa Baffoussam.

Wengi wa walioathirika na janga hilo ni waliojenga makazi kwenye maeneo hatarishi pembezoni mwa mlima ikiwa ni kinyume cha sheria za nchi hiyo.

Mvua kubwa zimeendelea kunyesha kwa siku kadhaa nchini humo, pamoja na nchi jirani kama vile Jamhuri ya Afrika ya Kati na Nigeria.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Zoezi la uchukuaji wa fomu kwa Wagombea ngazi ya serikali za mitaa.

Read Next

Mafuriko Nchini Somalia, Watu 182,000 wakosa Makazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!