Hakikisheni Vijiji vinafanikiwa na Mawasiliano.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewataka wadau wa sekta ya elimu na mawasiliano hapa nchini kuweka mazingira wezeshi na njia mbadala ya kuimarisha huduma ya upatikanaji wa mawasiliano kwa wote katika taasisi zote za elimu maeneo ya vijijini ambayo hayajafikiwa na huduma hizo.

Prof. Ndalichako amesema hayo jijini Dodoma akimwakilisha waziri mkuu katika kongamano la 4 la kimataifa la huduma za mtandao jamii liloshirikisha nchi zaidi ya sita kutoka Afrika pamoja na bara la Ulaya na kueleza kuwa ili kuwezesha taifa kufikia uchumi wa kati kuna kila sababu ya kuwekeza kwenye sekta ya mawasiliano kwa wote.

Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma UDOM Prof. FAUSTINE BEE amesema lengo lao ni kuzifikia taasisi zote ambazo huduma za mitandao jamii hazijafika na kuiomba serikali isaidie kutatua changamoto zinazozuia utekelezaji wa azma hiyo.

Baadhi ya wadau wa sekta ya mawasiliano kutoka mataifa mbalimbali wamesema kupitia huduma ya mitandao jamii itawezesha kufikia idadi kubwa ya wananchi hususani katika maeneo ambayo huduma ya mtandao jamii haijafika.

Comments

comments

clement

Read Previous

Wakulima Kilwa waliotapeliwa Fedha zao warejeshewa.

Read Next

Zoezi la uchukuaji wa fomu kwa Wagombea ngazi ya serikali za mitaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!