ALSF na AfDB zimekubaliana kuandaa mafunzo maalum ya msaada wa kisheria.

Tanzania na Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyo chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimekubaliana kuandaa mkakati maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada wa kisheria kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP) hususani katika kusimamia mashauri katika mahakama na mabaraza ya usuluhishi ya Tanzania na ya Kimataifa katika maeneo ya madini, biashara na usuluhishi na makampuni ya Kimataifa pamoja na mafuta na gesi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo mara baada ya majadiliano na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) Bwana Stephen Karangizi mazungumzo yaliyofanyika katika makao makuu ya Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Abidjan Nchini Ivory Coast.

Prof. Kabudi amesema kuwa lengo la majadiliano hayo ni kuisaidia Tanzania kuweka mikakati kuimarisha sekta ya Sheria ikiwa ni pamoja na kuiongezea uwezo ofisi ya mwanasheria mkuu wa Tanzania hasa baada ya mabadiliko makubwa yaliyofanywa ya muundo mpya wa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ili kuiwezesha kutoa ushauri wa kina na wa kitaalam kwa serikali lakini pia kusimamia mashauri katika mahakama na mabaraza ya usuluhishi ya Tanzania na ya Kimataifa.

Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyo chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ilianzishwa kutokana na ombi la Mawaziri wa fedha kutoka Afrika kwa lengo la kuzisaidia Nchi za Afrika kujijengea uwezo katika masuala ya kisheria hususani katika madini, mafuta na gesi pamoja na madeni ili kuziwezesha kuwa na uwanja sawa wa majadiliano katika ngazi za Kimataifa kuhusu biashara na makampuni ya Kimataifa.

Comments

comments

clement

Read Previous

Spika Ndugai amezitaka nchi za Kiafrika kuondokana na lugha za Wakoloni.

Read Next

TAKUKURU yawashikilia Wafanyabiashara wa Kichina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!