CCM imewataka wanachama wake kuhakikisha wanakiimarisha Chama hicho.

Chama Cha Mapinduzi CCM kimewataka wanachama wake kuhakikisha wanakiimarisha Chama hicho kwa kujitolea kwa hali na Mali kuanzia ngazi za Matawi ili kiendelee kuwa madhubuti na kujiandaa na Ushindi kuanzia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 24 hadi uchaguzi Mkuu 2020.

Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ali akizungumza na waandishi wa habari jijini Dsm amesema Agizo hilo ni Miongoni Mwa Maazimio yaliyotolewa katika kikao cha Kamati kuu kilichokutana hivi karibuni chini ya M/kiti wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Aidha Dkt. Bashiru amesema Miongoni Mwa Maazimio mengine ya Kamati Kuu ya CCM ni Pamoja na Kuimarishwa kwa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na chama Cha Mapinduzi.

Aidha Dkt. Bashiru amewataka wanachama wa CCM kuhakikisha wanakitumikia chama chao na Kukilinda pamoja na kulinda mali zake lakini pia akasisitiza kuongeza nguvu katika Mfumo mpya wa kadi za uanachama kwa njia ya Kieletroniki.

Comments

comments

clement

Read Previous

Saluni Dar es Salaam zajihusisha na Biashara ya Vipodozi vilivyopigwa marufuku.

Read Next

Miaka Minne ya Mhe. Rais Dkt. Magufuli madarakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!