Miaka Minne ya Mhe. Rais Dkt. Magufuli madarakani.

Ikiwa imetimia miaka minne ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, baadhi ya wakazi wa mkoa wa Rukwa wameeleza baadhi ya kazi alizozifanya Rais katika awamu ya Tano ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM lakini pia ni utekelezaji wa maendeleo kwa wananchi wa mijini na vijijini.

Nchi nzima inang’ara kwa vituo vya afya takribani mia nne, bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa CHF, lengo likiwa ni kuimarisha mifumo ya utoaji huduma ya afya kwa wananchi wenye kipato cha chini, hivi sasa maisha ya kijijini na mijini hayana pengo kubwa kutokana na upatikanaji wa nishati ya umeme kila mahali.

Pamoja na kuwajibika kwa mambo ya jumla katika jamii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa kimbilio la wengi hata wenye shida binafsi kama anavyowasilisha shukrani zake kwa Rais mama mjane Felister Mkombo mkazi wa wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.

Comments

comments

clement

Read Previous

CCM imewataka wanachama wake kuhakikisha wanakiimarisha Chama hicho.

Read Next

Kuelekea mechi ya soka ya ZEINI ICE-CREAM Football Club na timu ya AMGL FC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!