Saluni Dar es Salaam zajihusisha na Biashara ya Vipodozi vilivyopigwa marufuku.

Baadhi ya saluni za kike zilizopo jijini Dar es Salaam zimebainika kuendesha biashara ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kutokana na kuwa na viambata vya sumu.

Ukaguzi uliofanywa na Shirika la Viwango Tanzania TBS kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, umebaini baadhi ya saluni hizo katika eneo la Mwenge, ambako sampuli za vipodozi hivyo vimekamatwa baada ya kuthibitishwa kwenye maabara za shirika hilo kwamba havifai kwa usalama wa afya ya mtumiaji.

Mkaguzi mwandamizi wa TBS Mhandisi Donald Manyama amewaambia waandishi wa habari kuwa, biashara hiyo inafanyika kwa kificho ambapo wamiliki wa saluni hizo hawana leseni za kufanya mauzo ya vipodozi.

Aidha Mhandisi Manyama ameeleza kuwa, uchunguzi wao umebaini pia kuwa vipodozi vingi ambavyo haviruhusiwi kwa matumizi ya binadamu ni vile ambavyo vinaingizwa kutoka nje ya nchi kwa njia zisizo halali.

Comments

comments

clement

Read Previous

Rais Dkt. Magufuli aagiza wizara ya fedha kutoa Bilioni 40.

Read Next

CCM imewataka wanachama wake kuhakikisha wanakiimarisha Chama hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!