Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Leo ikiwa ni siku ya mwisho ya kurudisha fomu kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa, Serkali imewataka wale wote wenye malalamiko kutumia siku ya kesho yaani tarehe 5 na 6 kuwasilisha kwenye mamlaka husika ili yaweze kufanyiwa kazi.

Pazia la kuchukua na kurejesha fomu lilifunguliwa Oktoba 29 mwaka na kukamilika Novemba 4 mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi, tarehe 5 ni siku ya uteuzi wa wagombea na tarehe 6 ni siku ya kuwasilisha malalamiko ama mapingamizi kwa wale ambao hawakuridhishwa na mchakato huo ambapo mamlaka husika zitatoa maamuzi kuhusu mapingamizi hayo tarehe 6 hiyo hiyo.

Channel Ten imezungumza na mgombea wa mtaa wa Mpakani kata ya Ndugumbi Saleh Kawambwa anayetetea kiti chake ambaye anasema kwa upande wake amechukua fomu yeye na wajumbe wake na kuzirejesha kwa wakati na leo wamepata nakala za fomu kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi wa kata hiyo.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Selamani Jafo amekwisha tangaza ratiba kwa wagombea kuwasilisha mapingamizi pamoja na malalamiko ambayo yatapatiwa ufumbuzi kuwezesha uchaguzi kufanyika kama ilivypangwa na kwamba ofisi yake imepokea malalamiko kutoka mikoa mbalimbali ambapo jumla ya kata 72 kati 3956 ndizo zimekuwa na dosari sawa na asilimia 1.8 ya maeneo yote.

Uchaguzi huu umetajwa kuwa ndio dira ya uchaguzi mkuu ujao hivyo kila mwananchi anaombwa kujitokeza kutumia haki ya kuchagua kiongozi anayemtaka kwa kupiga kura.

Jumla ya watanzania milioni 19.6 wamejiandikisha kwenye daftari kwa kudumu la wapiga kura kati ya milioni 22.9 sawa na asilimia 86 ya lengo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Watendaji Wakuu na Wataalam Sekta ya Afya SADC wakutana.

Read Next

Tusimamie Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa Uchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!