Mvutano kati ya Salva Kiir na Riek Machar wazua wasiwasi.

Tofauti kubwa iliyopo kati ya mahasimu wawili wa Sudan Kusini, rais Salva Kiir na kiongozi mkuu wa upinzani Riek Machar, inatishia kuitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro mwingine, wakati huu wa kueleka kuunda kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa hivi karibuni.

Imeelezwa kuwa Mvutano uliopo baina ya Viongozi hao ikiwa hautatafutiwa suluhu ndani ya takribani wiki moja iliyosalia, huenda ukaitumbukiza Sudan Kusini katika mgogoro mkubwa wa kikatiba na hata kurejewa kwa mapigano baina ya pande hizo mbili.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na mataifa kadhaa ya magharibi, wanazitaka pande hizo mbili kuhakikisha wanaunda Serikali ndani ya muda uliopangwa.

Raia wa Sudani Kusini wana wasiwasi ya kuzuka mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na kusababisha vifo na umati wa watu kurudi kuyahama makaazi yao kama ilivyotokea katika miaka ya hivi karibuni.

Tayari Riek Machar amesogeza mbele mara kadhaa tarehe ya kurudi kwake nchini Sudani Kusini ambapo kiongozi huyo alitarajiwa kurudi jijini Juba nchini Sudan Kusini mwezi Mei mwaka huu.

Comments

comments

clement

Read Previous

Rais Dkt. Magufuli amuapisha CAG Mpya.

Read Next

Watendaji Wakuu na Wataalam Sekta ya Afya SADC wakutana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!