Rais Dkt. Magufuli amuapisha CAG Mpya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli leo amewaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni akiwemo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Edward Kichere pamoja na Majaji 12 wa Mahakama Kuu ya Tanzania na kuwataka Viongozi hao wapya kuwatumikia Watanzania na kutenda haki kwa wanyonge.

Aidha Majaji walioapishwa leo ni Dkt. Zainabu Diwa Mango, Edwin Elias Kakolaki, Dkt. Deo John Nangela, Fredrick Kapela Manyanda., Elizabeth Yoeza Mkwizu na Augustine Karichuba Rwizile.

Wengine ni Ephery Sedekia, Angaza Mwaipopo, Joachim Charles Tiganga, Kassim Ngukali Robert.
Said Mashaka Kalunde, na Bi. Angela Antony Bahati pamoja na Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti na Makamishna watano wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Akizungumza baada ya Kuwaapisha Viongozi hao katika Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar Es Salaam Rais Dkt. Magufuli amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa hesabu za Serikali kuisafisha Ofisi ya CAG na Taasisi zote za Serikali ikiwa ni pamoja na kuheshimu mipaka ya Mihimili Mikuu ya dola.

Awali Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Juma Ibrahimu Juma wamewataka Viongozi hao hususan majaji kutenda haki katika utekelezaji wa majukumu yao.

Comments

comments

clement

Read Previous

Kuelekea mechi ya soka ya ZEINI ICE-CREAM Football Club na timu ya AMGL FC.

Read Next

Mvutano kati ya Salva Kiir na Riek Machar wazua wasiwasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!